Michezo

Utata mtupu hatma ya wanariadha wa kike wenye homoni nyingi za kiume

Utafiti mpya unasema kuwa wanawake wanaozaliwa na viwango vya juu vya homoni za kiume {Testosterone} wana uwezo mkubwa wa utendaji ukilinganisha na wasichana wenzao katika mashindano.

Mwanariadha wa Africa Kusini, Caster Semenya akiwa katika mbio za wanawake mita 800

Ripoti hiyo iliyochapishwa katika jarida la matibabu michezoni inatokana na sampuli 100 za damu zilizochukuliwa kutoka kwa wanariadha katika kipindi cha miaka miwili.

Imechapishwa wiki chache kabla ya mahakama ya usuluhishi kuhusu maswala ya michezo kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu Shirikisho la wanariadha duniani I.A.A.F kuwapiga marufuku wanariadha wa kike walio na homoni nyingi za kiume. Marufuku hiyo iliyotolewa mwaka 2011, ilisitishwa na mahakama hiyo miaka miwili iliyopita.

Watafiti wake wanasema kuwa ushirikiano kati ya viwango vya juu vya homoni za testosterone na utendaji bora haufai kuchukuliwa kama kithibitisho.

By Hamza fumo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents