Habari

Utawala wa miaka 30 wa Omar al-Bashir Sudan kufikia kikomo leo ? Jeshi lasubiriwa kutoa tamko

Utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir umegubikwa na mapigano. Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameiongoza taifa hilo kubwa zaidi Afrika kwa mkono wa chuma hadi mwaka 2011. Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini.

Tuhuma dhidi ya Omar al-Bashir

Mauaji ya kimbari

  • Kuwaua watu wa jamii ya Fur, Masalit na Zaghawa
  • Kuwasababishia mafadhaiko makubwa ya kimwili na kiakili
  • Kuwaweka katika hali ngumu kwa kuwaharibia makaazi yao

Uhalifu dhidi ya binadamu

  • Mauaji
  • Kumpoteza mtu
  • Kuwahamisha watu kwa nguvu
  • Ubakaji
  • Mateso

Uhalifu wa kivita

  • Kushambulia raia katika jimbo la Darfur
  • Kuiba mali katika miji na vijiji

Kwa picha: Waandamanaji na Wanajeshi Khartoum

Kwa mujibu wa BBC. Uhusiano kati ya waandamanaji na jeshi huenda ukabaini hatma ya maandamano ya dhidi ya rais Omar al-Bashir.

Picha hizi kutoka mitaa ya mji mkuu wa Khartoum yanatoa taswira kuhusu uhusiano huo.

Hapa, wanajeshi na waandamanji wanaonekana wakiwa karibu wakiwa nje ya makao rasmi. Na hakuna hisia ya uhasama baina yao.

Hapa, wanajeshi na waandamanji wanaonekana wakiwa karibu wakiwa nje ya makao rasmi. Na hakuna hisia ya uhasama baina yao.

Waandamanaji wamekuwa wakielekea katika makao makuu ya wizara ya ulinzi Khartoum
Wanajeshi wanaonekana nje ya makao makuu ya wakilinda lango kuu huku raia wakiandamana
Wanajeshi wameonekena katika njia ya maandamano, wakitazama kutoka juu ya mapaa ya nyumba, huku bunduki zikiwa zimeinushwa.
waandamanaji wawasalimia maafisa kwa shangwe

Kwa mujibu wa BBC Mpaka sasa hivi hakujakuwa na kauli yoyote mpaka sasa kutoka kwa jeshi nchini Sudan

Shirika la habari la Reuters kwa kutotaja duru, limeripoti kwamba rais Omar al-Bashir amejiuzulu na mashauriano yanaendelea kuunda baraza la mpito.

Tangu asubuhi jeshi limetarajiwa kutoa tangazo muhimu wakati maandamano yakirindima kwa siku ya sita mtawalia kumshinikiza rais Omar al Bashir ajiuzulu.

Umati mkubwa wa watu umekusanyika nje ya makao makuu ya jeshi katika mji mkuu Khartoum na waandamanaji wameapa kuondoka tu iwapo rais atajiuzulu.

Nyimbo za uzalendo zimekuwa zikichezwa katika redio ya taifa na uwanja mkuu wa kimataifa umefungwa sasa.

Shinikizo limeongezeka kutaka mageuzi ya kisiasa nchini .

Watu wamekuwa wakishereheka katika mji mkuu Khartoum na wito umetolewa kwa raia zaidi kujiunga katika maandamano hayo nje ya makao makuu hayo ya jeshi.

Picha kutoka eneo kuu la maandamano

Benjamin Strick, ni mwandishi wa BBC Africa Eye, amekuwa akitumia teknolojia kutambua uhalisi wa matukio katika maeneo katika kuthibitisha au kuhakiki picha zinazosemekana kutoka kwa waandamanaji Sudan.

Video hizi zinatoa taswira ya ukubwa wa hisia miongoni mwa waliokusanyika.

Raia nchini Sudan wanasubiri kwa hamu kile ambacho vyombo vya hanari vya kitaifa vinaeleza kuwa ni tangazo muhimu kutoka kwa jeshi.

Kumeshuhudiwa maandamano ya miezi kadhaa ya umma ya kumshinikiza rais al-Bashir ajiuzulu.

Uvumi umeenea kwamba huenda Omar al Bashir akajiuzulu, lakini hakujakuwa na taarifa rasmi mpaka sasa.

Huku maelfu ya waandamanaji wakikusanyika katika mji mkuu Khartoum, magari ya jeshi yanaripotiwa kuzifunga barabara kuu na matangazo ya redio yamekatizwa badala yake kumewekwa nyimbo za uzalendo.

Waandalizi wa maandamano wametoa wito kwa raia wasalie mitaani; wandishi habari wanasema wengi wataridhika tu iwapo serikali nzima ya Sudan itaondolewa, na sio rais tu.

Jeshi la Sudan limetangaza kuwa litatoa taarifa muhimu hivi karibuni, hali inayohisiwa kuwa utawala wa Rais Omar al-Bashir huenda ukafikia kikomo hivi karibuni.

Wanajeshi wametanda katika makazi rasmi ya rais mapema asubuhi ya leo, shirika la Habari la kimataifa la AFP linaripoti.

Jeshi pia limezingira njia zote muhimu za kuingia na kutoka mji mkuu wa Khartoum.

  1. eshi la Sudan limekuwa na jukumu kuu katika siasa za nchi hiyo tangu lilipojinyakulia uhuru mnamo 1956. Jeshi limeshutumiwa kwa kutumia vibaya malalamiko yanayowasilishwa kujipatia madaraka na alafu kuidhinisha utawala wa kukandamiza unoishia kugeuka matakwa ya raia.Mnamo 1958, miaka miwili baada ya uhuru, mkuu wa majeshi Meja Jenerali Ibrahim Abboud alichukua uongozi katika mapinduzi ambayo hayakukumbwa na umwagikaji damu. Vuguvugu lililokuwa maarufu lilishinikiza jeshi kuachia madaraka mnamo 1964.Jeshi baadaye lilirudi uongozini katika mapinduzi mengine mnamo 1969 yalioongozwa na Kanali Jaafar el-Nimeiri. Nimeiri mwenyewe aliidhinisha majaribio kadhaa ya mapinduzi na vuguvugu dhidi ya utawala.Mnamo 1985, Luteni – Jenerali Abdel Rahman Swar al-Dhahab aliongoza kundi la maafisa wa jeshi katika kumpindua el-Nimeiri.Mwaka mmoja baadaye, al-Dhahab alikabidhi madaraka kwa serikali iliyochaguliwa, ya waziri mkuu al-Sadiq al-Mahdi.Lakini miaka mitatu baadaye, mnamo 1989, maafisa wa kijeshi wenye itikadi kali za dini ya kiislamu walioongozwa na Brigedia Omar al-Bashir waliupindua utawala ambao haukuwa imara wa Al-Mahdi.Miaka 30 baadaye hii leo, Bashir amesalia uongozini, akiwa amekabiliwa na changamoto si haba katika utawala wake.Article share tools
  2. Imepakiwa mnamo 11:3111:31’Magari ya kijeshi yaingia katika makao ya rais Bashir’ nchini SudanMagari kadhaa ya kijeshi yameingia katika eneo ambako kuna makao makuu ya wizara ya ulinzi na makaazi rasmi ya rais Omar al Bashir, mapema leo alfajiri, shirika la habari la AFP limenukuu watu walioshuhudia hilo ambao hawakutajwa majina


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents