Habari

Utazama au Utaogelea? Kazi ni kwako

Kizazi cha vijana tunaotaka maisha mazuri bila subira, tukijaribu kufanya hili na lile kuhakikisha maisha yaende sawa na kwa kasi zaidi kifedha na kumiliki magari mazuri. Ni baaada ya kuelewa vibaya mafanikio ni nini? Mji wa Roma haukujengwa kwa siku moja, na sisi tunataka kuujenga kwa masaa machache? Inawezekana kama itakuwa muujiza , ila tunaishi maisha feki.

Woman experiencing stress

Uzame au Uelee kazi ni kwako. Twende kwenye mambo ya msingi. Akili ni nywele kila mtu ana zake, wakati msingi wa maisha ya mwanadamu ni mmoja kwahiyo tunatoka sehemu moja, kazi ni msingi wa kila kitu. Ninapozungumzia kazi simaanishi walioajiriwa peke yake, namaanisha wafanyabiashara, wakulima, wachoraji, wasusi na wapiga debe , na hata dobi.

Ukichanganyikiwa usiogope kuniuliza. Kuna mambo ya msingi ambayo tunatakiwa kujua na moja wapo ni kuwekeza. Hakuna mtu aliyeweza kufanikiwa bila kuwekeza isipokuwa mla rushwa, mwizi na wanaofanya biashara chafu ila nao wanawekeza uchafu wao. Ukiniona leo naendesha Benz kwa mfano halafu nimemaliza chuo juzi juzi, utajiuliza maswali mengi sana ila kama natokea familia yenye fedha hautashangaa.

Swali ni kwamba je umewekeza nini? Na umewekeza kwa kiasi gani kwenye jambo unalolifanya? Je biashara yako imeanza lini na unataka itoe faida kubwa na matokeo makubwa? Kila biashara ina mahesabu yake na muda wake wa kurudisha mtaji, watu wengi tumekuwa tukifanya biashara bila kujua na kuweka bei kubwa kubwa tukitaka mtaji urudi kesho yake. Biashara haiendi hivyo, jaribu kuangalia unachukua mzigo kiasi gani labda kwa mwezi, gharama ni kasi gani, kodi ya mwezi ni kiasi gani, mshahara ni kiasi gani, umeme na maji ni kiasi gani? Je utapata faidakiasi gani au ninataka faida iwe kiasi gani.

Namna ya kujua gharama za kibiashara, kama umenunua mashati kwa shilingi 3000 na yako mia, kodi ya pango ni 150,000/- maji na umeme ni 30,000/- na mshahara ni 150,000/-. Hivyo basi tunazungumzia gharama ya mashati 100 ni shilingi 630,000/- yakiuzwa kwa mwezi mmoja. 630,000/100 inamaanisha kurudisha hela yako ni kila shati kuuzwa shilingi 6300/-, Hivyo basi nikitaka nipate faida ya asilimia hamsini nitauza sharti hilo kwa angalau shilingi elfu kumi. Swali ni kwamba unajua namna ya kupanga bei ya bidhaa zako ili ziuzike? Unapataje Bei ya Bidhaa yako ili iingie sokoni? Huu ni wakati wa wewe kuongeza ujuzi katika taaluma yako ya biashara, soko limebadirika na unahitajika uwe makini na mwenye kujua ushindani ukoje.

Ninazungumzia taaluma ya biashara nyingi hapa Bongo hatuna ujuzi wa kujua gharama na kupanga bei ndo maana, tunabidhaa nyingi dukani haziuziki kwa sababu ya kutaka faida kubwa. Maduka mengi kama Kinondoni, Kijitonyama na Sinza  yanapata shida kukua kwa kasi kwa kuwa wanafanya biashara kizoefu. Itazame biashara yako kwa upya na ufanye unachostahili kufanya, haufanikiwi kwa kuuza bei kubwa bali kwa kupata wateja wengi ambao watarudi tena kwako wakati mwingine. Je taaluma yako ni biashara? Amua kuzama au kuelea kazi ni kwako. Watu wa Kariakoo WANAWEZA KUWA WANAJUA SIRI HII, kwa wafanyakazi nitarudi kwenu wakati mwingine.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents