Burudani ya Michezo Live

Uturuki yaanza kuwarejesha makwao wapiganaji wa kundi la IS, Mmarekani akwama mpakani – Video

Uturuki yaanza kuwarejesha makwao wapiganaji wa kundi la IS, Mmarekani akwama mpakani - Video

Raia wa Marekani aliyeshukiwa kuwa mwanamgambo wa Isalamic State amekwama katika mpaka wa Ugiriki na Uturuki, baada ya Uturuki kumfukuza.

Mshukiwa huyo alisafirishwa siku ya Jumatatu wakati Uturuki ilipoanzisha mpango wa kuwarejesha wapiganaji wa jihadi waliokuwa wakishikiliwa kwenye magereza.

Polisi nchini Ugiriki wamesema walimkatalia kuingia alipojaribu kuvuka mpaka karibu na mji wa Kastanies nchini Ugiriki.

Mwanaume huyo anaripotiwa kukwama kwa siku mbili katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.

Ametajwa na Shirika la habari na Uturuki kuwa Muhammed Darwis B na kusema kudaiwa kuwa raia wa Marekani mwenye asili ya Jordan.

Afisa wa Uturuki ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kuwa alikataa kurudishwa Marekani na badala yake aliomba apelekwe Ugiriki.

Mustakabali wa wapiganaji wa IS limekuwa swali muhimu tangu kudhibitiwa kwa kundi hilo kwenye maeneo waliokuwa wakidhibiti nchini Syria na Iraq.

Raisi a Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ameeleza kuwa wanamgambi 2,500 wako gerezani nchini Uturuki.

Zaidi ya nchi 70 ziliungana kupambana na kuangusha utawala wa jihadi nchini Iraq na Syria. Lakini kwa kampeni nyingine katika eneo la Mashariki ya kati, walishindwa kupanga ipasavyo jinsi ya kuyakabili matokeo.

Kutokana na mapigano ya mwisho dhidi ya IS katika mji wa Baghuz nchini Syria mwezi Machi, maelfu ya wapiganaji wa IS na wategemezi wao waliposhikiliwa kwenye makambi. Uturuki ambayo imekuwa ikiwakamata wafuasi wa IS kwa miaka kadhaa, sasa ina takribani wafuasi 2,000 wa IS.

Uturuki, Iraq na mamlaka za kikurdi wote wanataka Ulaya na nchi za magharibi kuharakisha kuwachukua raia wao lakini mpaka sasa serikali zimesita kufanya hivyo, moja ya sababu ni hofu ya kushindwa kuwashtaki.

 

Wizara ya mambo ya ndani imesema pia imerudisha raia wa Denmark mtu anayedaiwa kuwa mfuasi wa IS siku ya Jumatatu. Mamlaka ya Denmark imesema raia wake alikamatwa alipowasili mjini Copenhagen.

Ujerumani imesema mmoja wa raia wake pia alifukuzwa.

Uturuki imesema washukiwa 20 wenye asili ya Ulaya, wakiwemo raia 11 wa Uaransa, wawili wa Ireland na kadhaa wa Ujerumani, wako katika mchakato wa kurudishwa kwenye nchi zao.

Uturuki imezishutumu nchi za magharibi kwa kushindwa kuwajibika kwa raia wao waliojiunga na wanamgambo wa IS

Ujerumani,Denmark na Uingereza wamewavua uraia watu kwa madai ya kujiunga na makundi ya Jihad nje ya nchi zao, zikiwa ni hatua za kuwazuia kurudi.

Uingereza imesema imewavua uraia zaidi ya watu 100.

Siku ya Jumanne katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres aliomba ushirikiano kutatua matatizo yanayohusu wapiganaji wa kigeni, akisema haikuwa juu ya syria na Iraq kutatua tatizo kwa ajili ya kila mtu.

Hapo awali umoja wa mataifa uliwahi kusema nchi zinatakiwa kuchukua jukumu la raia wao isipokuwa tu kama wakishtakiwa ndani ya nchi zao, sawa sawa na viwango vya kimataifa.

Askari wakiwasindikiza wanawake wanaodaiwa kuwa wake wa wapiganaji wa ISAskari wakiwasindikiza wanawake wanaodaiwa kuwa wake wa wapiganaji wa IS

Uturuki haijathibitisha kama waliorudishwa walikamatwa nchini Syria au katika eneo la Uturuki.

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha IS na ndugu zao walikamatwa kaskazini mashariki mwa Syria mwezi October, pale Uturuki walipoanzisha msako katika mipaka kupambana na vikosi vya Kurdi vinavyoongozwa na vikosi vya demkorasia vya Syria.(SDF)

Kwa wakati huo, the SDF walisema kuwashikilia zaidi ya watu 1,200 wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha IS ndani ya magereza saba katika eneo hilo, huku watu 4,000 wakidhaniwa kutoka katika nchi za nje.

Wanaodhaniwa kuwa ndugu wa wanamgambo wa IS pia walikuwa wanashikiliwa katika kambi mbali mbali za watu walioyakimbia makazi yao, wengi wao wakiwa ni al-Hol ambao wnahudumia watu karibia 70,000.

Kwa mujibu wa BBC. Chanzo kutoka wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa kiliiambia shirika la habari AFP wiki iliyopita kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Jihadi walirudishwa nchini Ufarasa kutoka Uturuki chini ya makubliano ya mwaka 2014.

”Jihadi na familia zao mara kwa mara wanarudishwa Ufaransa na kukamatwa pale wanaposhuka kutoka ndani ya ndege. Muda mwingi hufanywa kwa siri. Habari hizi hazichapishwi wala kuachiwa wazi hapo baadae”, alisema mtu huyo ambaye hakutaka kujulikana.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW