Uwanja wa Taifa huenda ukafungwa

Uwanja wa Taifa huenda ikafungwa
Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imesema huenda ikalazimika
kusimamisha matumizi ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi pale
atakapopatika mzabuni wa kuuendesha

Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Florens Turuka alisema kuwa uamuzi huo unaweza kufikiwa kutokana na serikali kutumia gharama kubwa za uendeshaji wake tofauti na mapato yanayoingia.

"Tunaweza kusimamisha kabisa matumizi ya Uwanja wa Taifa mpaka hapo mzabuni atakapopatikana, hii inatokana na serikali kutumia fedha nyingi za uendeshaji wake huku mapato yanayopatikana hayatoshelezi,"alisema.

Alisema kuwa wizara yake inashangazwa na mapato kidogo yanapopatikana uwanjani hapo licha ya mashabiki wengi kuonekana kuhudhuria mechi hali inayowapa wasiwasi kuwa huenda kuna namna fulani ya hujuma inayofanyika kwa manufaa ya watu wachache.

"Unajua kuona ripoti ya mahudhurio ya watu ikiwa juu halafu mapato yanayopatikana ni madogo, hilo linatupa wasiwasi labda kuna hujuma fulani inayofanyika na ndio maana tunataka apatikane mzabuni tutakayemkabidhi mamlaka ya kusimamia ili uwanja uwe ni kwa faida ya umma na si watu wachache,"alisema Dk Turuka.

Dk Turuka alisema kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni kumalizika kwa muda wa zabuni iliyotangazwa ili waweze kupitia majina ya waombaji na kuangalia sifa zinazotakiwa kabla ya kumtangaza aliyeshinda.

Katika hatua nyingine, DkTuruka alisema kuwa leo anatarajia kuutembelea uwanja huo ili kuangalia kama kuna kasoro yoyote ili ziweze kurekebishwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents