Michezo

Uwezo wa timu za vijana wa ‘Magnet Youth Sports Organization’ wamkosha Sol Campbell (+Picha)

Mchezaji mkongwe wa klabu ya Arsenal, Sol Campbell amefurahishwa na uwezo wa timu za vijana wenye umri kati ya miaka 5  hadi 17, kwa kusema kama wakiongeza juhudi na kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja basi watafika mbali kwani wanauwezo mkubwa na wakustaajabisha.

Sol Campbell akijifua uwanjani na vijana wa MYSO

Sol Campbell ambaye yupo nchini Tanzania tangu Jumamosi tarehe 5 Agosti 2017, amesema vijana wanaonekana wenye nguvu na nia na wanauwezo na vipaji vya kufikia malengo yao huku akiwahimiza kuwa kama wanataka kufikia malengo yao hawana budi kuwaheshimu walimu wao na kujituma zaidi.

Ili uwe mchezaji bora au ufikie malengo yako inakupasa uwe na nidhamu ndani na nje ya uwanja kwani huwezi kufanikiwa kama utakuwa na utovu wa nidhamu cha pili ni kujituma kwenye mazoezi na kuweka nia ya kile unachokifa vitu kama juhudi kwenye mazoezi vitakufanya ufanikiwe naamini hapa kuna akina Campbell wengi nawaona tena wenye vipaji vikubwa”,amesema Sol Campbell mapema leo asubuhi alivyotembelea timu za vijana wa Magnet Youth Sports Organization kwenye viwanja vya Gymkhana.

Hata hivyo, Campbell amekutana na viongozi na wazazi wa vijana hao na kuwata waendelee kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu ili waweze kufikia malengo yao.

Kwa upande wake muanzilishi wa Academy ya Magnetic Youth Sports Organization, Juma Maswanya ameishukuru Kampuni ya kubashiri ya SportPesa kwa kusema wameonesha mwanga kwa mpira wetu hapa nchini ambao ulikuwa hauna nyuma wala mbele.

Tazama picha za Sol Campbell alivyowatembelea timu hizo za vijana.

Sol Campbell akipokelewa na CEO wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov kwenye viwanja vya Gymkhana.

Kocha wa timu ya vijana, Juma Maswanya akimpatia historia ya Academy ya MYSO

Sol Campbell na zawadi ya shuka la kimasai

Sol Campbell akiwa na timu za vijana

Sol Campbell na Wazazi wa vijana wa Academy ya M.Y.S.O

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents