Habari

Uzalendo ni muhimu – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wote wahakikishe wanaboresha mshikamano wao pamoja na kuimarisha uzalendo kwa Taifa lao huku akisema uzalendo ni muhimu sana.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Kitanzania wanaosomea udaktari nchini Cuba.

“Uzalendo ni muhimu sana kwa sababu tumekosa fursa nyingi za kimaendeleo kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao.”

Hata hivyo Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua uwepo wao wa kimasomo nchini Cuba na kwamba inatarajia kupata mchango mkubwa kutoka kwao punde wamalizapo masomo yao.“Nawaomba msome kwa bidii na mfaulu mitihani yenu. Elimu yenu iwasaidie katika ajira na muweze kurejesha mikopo mliyopewa na Serikali ili iwanufaishe wengine.”

Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao kuzingatia sheria za nchi waliyoko pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo yao.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents