Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Bongo Movie

Uzinduzi wa filamu ya Mr Kiongozi ya Odama kupambwa na Rayvanny

By  | 

Wakati tasnia ya filamu ikiwa kimwa kutokana na waigizaji wengi nchini Tanzania kusitisha kuachia filamu, Jenifer kyaka aka Odama katika siku kuu ya Eid pili mkoani Tanga ameandaa tamasha la uzinduzi wa filamu yake mpya Mr Kiongozi huku burudani ikitarajiwa kutolewa na msanii kutoka WCB, Raynanny.

Filamu hiyo imewakusanya mastaa wengi akiwemo Jacqueline Wolper, Hemed PHD, Mzee Hashim Kambi, Odama pamoja na mastaa wengine wangi.

Mwigizaji huyo amesema tamasha kupambwa na msanii Rayvanny pia mashabiki watapata fursa ya kupiga picha na mastaa mbalimbali kupitia red carpet pamoja na kubadilisha nao mawazo.

Pia alisema atatumia fursa hiyo kuzungumza na wasanii wa mkoa wa Tanga wenye malengo ya kutaka kufanya sanaa ili kuwaonyesha njia pamoja na kuwasaidia kwa wale ambao ataona wanahitaji msaada kupitia kampuni yake ya J Film.

Kwa upande wa muimbaji Rayvanny kutoka WCB amethitisha kutua mkoani Tanga kwaajili ya Tamasha hilo huku akiahidi kufanya mambo makubwa kwa kuwa ni mara chache sana kukutana na mashabiki wake wa mikoani.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW