Burudani

Uzushi kuwa Irene Uwoya amefariki wadaiwa kusababisha usumbufu mkubwa kwenye familia

Taarifa za uzushi zilizoandikwa jana kwenye Facebook kuwa muigizaji wa filamu, Irene Uwoya amefariki, zinadaiwa kusababisha usumbufu mkubwa kwenye familia yake.

11352128_823123387807063_106497935_n

Uzushi huo umekanushwa na kulaaniwa vikali na muigizaji mwenzake, Jacob Stephen aka JB.

“Ndugu zangu jana kupitia akaunti feki ya facebook kuna mtu alitoa picha yangu nikilia na kusema Irene Uwoya amefariki,” ameandika JB kwenye Instagram.

“Habari hii ya uongo ilileta shida kubwa katika familia yake na watu wa karibu. Leo tena asubuhi mwingine kasema nimepata ajali nakusababisha tafrani kubwa,” aliongeza.

“Napenda kuwaambia mashabiki wetu kuwa habari hizo ni za uongo. Tuko fiti kwa damu ya Yesu na tunavunja roho hizo za kunenea watu mabaya ktk jina la Yesu..amen.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents