Burudani

Valentine’s Day: Hizi ni rekodi 8 za Guinness za mambo ya mapenzi duniani

Harusi kubwa zaidi kuwahi kufungwa chini ya maji

Valentines Underwater-wedding_tcm25-371924

Harusi kubwa zaidi iliyowahi kufanyika chini ya maji ilihusisha watu 303 waliohudhuria harusi kati ya Ewa Staronska na Pawel Burkowski wa Poland. Ndoa hiyo ilifungwa August 27, 2011.

Ndoa iliyodumu kwa muda mrefu zaidi

Ndoa hiyo ni kati ya Herbert Fisher (aliyezaliwa 10 June 1905) na Zelmyra Fisher (aliyezaliwa 10 December 1907) wa Marekani ambao walifunga May 13, 1924 huko North Carolina, USA.

Waliendelea kuwa pamoja kwa miaka 86, miezi 9 na siku 16 hadi February 27, 2011. Herbert Fisher alifariki Jumapili hiyo. Walikuwa na watoto 5.

Boksi kubwa zaidi la Chocolate

110017-3325440_tcm25-19710

Hilo ni boksi la Thorntons Moments lenye uzito wa kilo 1,689 lililopimwa huko Bethnal Green, London, UK, April 2, 2008.

Shairi la mapenzi la zamani zaidi

Shairi la zamani zaidi la mapenzi ambao hadi leo lipo liliandikwa kwenye meza ya udongo enzi za Sumerians, wabunifu wa uandishi miaka ya 3500 BD. Shairi hilo lilisomeka:
Bridegroom, dear to my heart,

Goodly is your beauty, honeysweet,

Lion, dear to my heart,

Goodly is your beauty, honeysweet.

#swoon

Mkusanyiko mkubwa zaidi wa Teddy Bears

119084-8786402_tcm25-19711

Mpaka anahasehabu mara ya mwisho, Jackie Miley (USA) wa Hill City, South Dakota, alikuwa na teddy bears tofauti tofauti 8,026 alizoanza kuzikusanya tangu mwaka 2002.

Mchoro wa ukutani wenye busu nyingi zaidi

Largest-mural-of-kisses_tcm25-371996

Mchoro mkubwa wenye busu nyingi zaidi ulikuwa na alama za busu 13,316 zilizochorwa na NIVEA Brasil, kwenye Pinheiros Station, São Paulo, Brazil, June 12, 2012.

Mtu aliyekumbatia watu wengi zaidi ndani ya saa 24

Mtu aliyekumbatia watu wengi zaidi ndani ya saa 24 ni Jonathan Sexton wa Marekani, aliyewakumbatia watu 8,709 ndani ya muda huo kwenye tamasha la Bonnaroo Music and Arts Festival, Manchester, Tennessee, June 11, 2010.

Busu lililodumu kwa muda mrefu zaidi

139604-7838231_tcm25-19713

Busu hilo lilidumu kwa masaa 58, dakika 35 na sekunde 58 na lilifanywa na Ekkachai Tiranarat na Laksana Tiranarat wa Thailand kupitia Ripley’s Believe It or Not! February 12-14, 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents