Michezo

Van Gaal akana mambo kuwa magumu

Baada ya Newcastle United kumfukuza kocha wake Steve Mclaren, hali inazidi kuwa mbaya kwa Louis Van Gaal.

images

Ikiwa ni msimu wa pili tangu asajiliwe na United, hali imezidi kuwa ngumu kwa kocha huyo baada ya kufungwa kwenye mechi mbili mfululizo na ikiwa inashika nafasi ya tano kwenye kombe la ligi kuu ya Uingereza (EPL).

Baada ya kufungwa na mahasimu wao wa muda mrefu timu ya Liverpool, Van Gaal amesema, “Nadhani mbinu hiyo inafanya kazi,” akikana madai kwamba klabu hiyo imefeli katika uongozi wake.

“Hatupati matokeo mazuri sana. Sio mazuri sana ukifikiria kwamba ni lazima uwe bingwa wa ligi, ushinde kombe la bara Europa ama upate ushindi wa kombe la FA. Kuna wenzetu wengi ambao hawapiganii makombe matatu.”

Manchester United wataikaribisha Westham United uwanja wa Old Trafford siku ya Jumapili kwenye kombe la FA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents