Burudani
Vanessa, Izzo B, Quick Rocka na wengine kumsindikiza Jux kwenye uzinduzi wa video yake Jumapili hii
Vanessa Mdee, Izzo B na Quick Rocka ni miongoni mwa wasanii kibao watakaomsindikiza muimbaji wa kundi la Wakacha, Jux kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake Uzuri wako.
Wengine ni pamoja na Cyril aka Kamikaze, Mirror, Samir na Rich Mavoko. Uzinduzi huo utafanyika Jumapili hii ya Sept 1 kwenye ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam ambapo pia Jux atazindua wimbo wake mpya.
Host wa tukio zima atakuwa mtangazaji wa Clouds FM, B12.