Burudani

Vanessa Mdee aelezea sababu za kushindwa kufanya kipindi cha ‘The One Show’ ya TV1

Jana (March 12) kituo kipya cha televisheni TV1 Tanzania kilizinduliwa rasmi jijini Dar es salaam, sambamba na show yao mpya iitwayo ‘The One Show’ itakayoendeshwa na watangazaji wawili Jokate Mwegelo na Ezden Jumanne, badala ya Vanessa Mdee aliyeonekana katika picha za maandalizi ya awali ya kipindi hicho.

Vanessa

Kwa mujibu wa Millardayo.com mtangazaji huyo wa kituo cha redio Choice FM ametoa sababu za kushindwa kufanya kipindi hicho kama ilivyokuwa inatarajiwa.

“V money anapenda kukufahamisha kwamba hatoonekana kwenye show hiyo, yani hajaichukua hiyo kazi kutokana na ratiba yake (V) kumbana kutokana na mipango yake ya sasa pia ya kusafiri kuendeleza muziki wake.” Hivi ndivyo mtandao huo umeripoti.

Vanessa ambaye pia ni msanii anafanya vizuri na single yake ya sasa ‘Come Over’, ambayo mwishoni mwa mwaka jana aliweza kui-perform katika show inayowakutanisha mastar wa muziki nchini Nigeria kila mwaka ‘Rhythm Unplugged’, ambayo kwa mwaka jana host alikuwa Wyclef Jean.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents