Habari

Vanessa Mdee ajibu tuhuma za kutohudhuria kwenye misiba ya hivi karibuni

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Vanessa Mdee ameshindwa kuvumilia na kuamua kujibu baadhi ya watu wanaomuandama kuwa haudhurii kwenye misiba.

Vanessa Mdee

Vanessa amejibu tuhuma hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kudai kuwa amekuwa akihudhuria lakini kimya kimya kwani misiba na mazishi ni ibada na hakuna umuhimu kujionesha.

“Niliona nipotezee lakini naomba niseme once and for all. Misiba na mazishi ni kama ibada, ukishiriki sio habari ya kutangaza kama tamasha. Nimeona watu wanataka kunishikilia bango kama mtu asiyehudhuria au asiyeshiriki katika ibada hizi. Kama unataka kufaham nilikuwepo katika misiba yote ya hivi karibuni lakini sikupenda kutangaza uwepo wangu kutokana na kupitia misiba mizito katika maisha yangu kama watu wengine wengi. Siku ya kesho itakuwa miaka 12 tangu nimpoteze baba yangu mzazi na mwaka huu ni miaka miwili tangu nimpoteze Dada yangu ( mtoto wa kwanza wa baba) i bet you didn’t even know, why? Because I prefer to silently pray for the family and loved ones, I’ve found that only God can bring some relief in these situations. “ameeleza Vanessa Mdee na kufafanua.

Mtu akifiwa anapitia mambo mengi na anahitaji faraja. Nadhani nimeeleweka. Asanteni na Mungu awatunze wote na familia zenu.

Kwa wiki tatu mfululizo, Tanzania imekumbwa na misiba ya watu maarufu kwenye tasnia ya habari na burudani, ikiwemo msiba wa Rapper Godzilla, Mtangazaji wa clouds FM, Ephraem Kibonde na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents