Burudani

Vanessa Mdee alikuwa ameandaa wimbo mbadala kama watanzania wangeshindwa kuielewa ‘Nobody But Me’

Vanessa Mdee amesema wakati anauachia wimbo wake Nobody But Me ambao kwa sasa ni hit ya Afrika nzima, alikuwa ana wasiwasi iwapo watanzania wataulewa.

Akiongea na Bongo5, Vanessa aliyetajwa kuwania kipengele cha msanii bora wa kike kwenye tuzo za MTV MAMA amesema kutokana na wasiwasi huo alikuwa ameshatayarisha wimbo mbadala wa kuutoa.

Anasema Nobody But Me ni wimbo alioutoa kwaajili ya kimataifa zaidi lakini ameshangaa kuona umekubalika mno nchini pia.

“Nilikuwa na wasiwasi sana sio kidogo,” amesema Vee. “Na nilikuwa nimeshatayarisha nyimbo ya nyumbani. “Nilikuwa naiamini, naijua na nailewa na ndio maana nimeshoot video na nimewekeza pesa nyingi kwenye hiyo nyimbo lakini nilikuwa nasema just incase ikatokea kwamba nyumbani hawataipenda ninayo nyimbo ambayo ipo tayari kwaajili ya nyumbani. So nilikuwa naupa kama mwezi I am like let me just listen,” ameongeza.

Vanessa anasema pamoja na kujiamini kuwa anafanya muziki mzuri anaamini kuwa kama msanii hatoweza kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani hawezi kufika popote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents