Burudani

Vanessa Mdee asimulia alivyokuwa akitaniwa utotoni wakati akisoma Paris kutokana na umbo lake dogo

Vanessa Mdee amedai kuwa wakati anasoma shule jijini Paris, Ufaransa miaka mingi iliyopita wakati familia yake ikiishi huko, alikuwa akitaniwa na watoto wa kizungu kwakuwa alikuwa na umbo dogo.

14714417_1704175103234677_7148436871884832768_n

Amekumbushia kisa hicho kwenye mahojiano na mtangazaji wa BBC Radio Service , Salim Kikeke kwenye makala ya Kiingereza ya Global Beat: Tanzanian Hip hop.

“Nilikuwa nikitaniwa sana kwasababu nilikuwa mwembamba sana, nilisoma shule Paris na walikuwa wakiniita Msomali,” amesema Vee.

“Nilikuwa nikirudi nyumbani nalia na mama angeniuliza tatizo nini ningemwambia kilichotokea na unajua kuwa kwenye nchi ya kigeni na angesema ‘puuzia’ na mimi ningesema ‘unaamisha nini nipuuzie, nataka uende ukafanye timbwili shuleni’ unajua. Na asingefanya hivyo kamwe, angeniambia tu ‘puuzia’ sababu hapo ndio moyo wako halisi hujitokeza, huo ndio wajihi,” alisema Vanessa.

Vanessa anamaanisha kuwa hiyo ndio sababu aliandika wimbo wake Hawajui uliompa tuzo mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents