Tia Kitu. Pata Vituuz!

Vanessa Mdee atangaza nafasi ya ajira ya ‘msaidizi wake mkuu’

Tunaposema muziki ni ajira hiki ndicho tunachokimaanisha, wasanii wa muziki na filamu wanapofanikiwa kutokana na shughuli zao za sanaa, pia wana nafasi ya kuwasaidia na vijana wenzao kwa kuwapa ajira kutokana na sanaa yao.

vee3

Vanessa Mdee ni brand inayoendelea kukua ndani na nje ya Tanzania, na ndio sababu muimbaji huyo wa ‘Never Ever’ ameamua kutoa nafasi ya ajira ya Msaidizi Mkuu (Personal Assistant).

Kupitia Instagram Vee Money amepost:

vee kazi

Hili ni jambo jema kufanywa na msanii, kwasababu kama ikitokea kila msanii akihitaji msaidizi kuna vijana wengi wenye vipaji na uwezo watakuwa wamepata shughuli za kufanya na kuwaingizia kipato kutokana na chanzo cha muziki au sanaa kwa ujumla.

Kama wewe ni kijana na unahisi una vigezo vya kuwa msaidizi wa Vee, tembelea website yake www.vanessamdee.com kupata maelekezo zaidi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW