Burudani

Vanessa Mdee atunukiwa tuzo ya ‘Nyota wa Mchezo’ baada ya kufanya vizuri 2017

Ikiwa ni wiki moja tu baada ya kuachia album yake ya kwanza, Money Mondays, Vanessa Mdee amekuwa msanii wa kwanza nchini kutunukiwa tuzo (plaque) ya Nyota wa Mchezo kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Vanessa Mdee akipokea tuzo NYOTA WA MCHEZO Plaque na The Playlist, Lil Ommy

Amepewa Plaque hiyo Jumatatu ya January 22 baada ya mwaka jana kutajwa na kituo hicho kuwa ndiye Msanii Bora wa Kike, Mtumbuizaji Bora, Mtumbuizaji Bora Jukwaani na Msanii Bora kuibuka katika mwaka (Emerging Artist of the Year).

“Imekuwa siku ya furaha tele kwangu mimi, imekuwa wiki ya furaha, mwezi wa furaha, mwaka wa furaha na nyie mmeniongezea furaha siku ya leo,” amesema Vanessa Mdee baada ya kupewa plaque hiyo.

“This plaque is amazing, ni ishara kwamba sometimes tunajisikia kama hamuoni au hamwelewi lakini mmeelewa na kuona na leo hii tumefikia hapa. Thank you to The Playlist na timu nzima ya Times FM and zaidi mashabiki kwa kunipa fursa hii because it’s been almost five years kwenye game na Money Mondays is legit finally tunayo album yetu and kiukweli I couldn’t have done this without you guys,” ameongeza.

Mtangazaji wa kipindi hicho, Omary ‘Lil Ommy’ Tambwe amesema ameanza kutoa plaque hiyo kwa kutambua mchango na mafanikio ya msanii na kazi nzuri aliyofanya. Amesema lengo ni kuwapa nguvu na kusherehekea mafanikio ya kazi za msanii na sanaa kwa ujumla Tanzania.

“Wazo la kutoa Nyota wa Mchezo lilianza mwaka jana mwishoni December ambapo nilitumia Twitter kutaja wasanii wengi kama Nyota wa Mchezo. Kutokana na kuelekea mwisho wa mwaka, ni bora kuwapongeza wale waliofanya vizuri katika sehemu zao kwenye burudani,” amesema Lil Ommy.

“Vanessa alikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kuandika tweet yake na wazo lilianzia baada ya kumfikiria yeye na kuona kazi nzuri alizofanya na baadaye nikaendeleza list ya watu wengi kwa hashtag ya #BongoFleva2017 #NyotawaMchezo na kutaja nafasi zao (vipengele) ambavyo wamefanya vizuri. Niliangalia impact (matokeo/athari) ya msanii, impact ya kazi zake, popularity (umaarufu), kujulikana, airplays (kazi yake kuchezwa kwenye radio na TV), views (watazamani kwenye YouTube), anavyozungumziwa kwenye mitandao ya kijamii, ubora wa kazi, ukuaji wa msanii, ukomavu wa msanii na kuwataja kama NYOTA WA MCHEZO” ameeleza.

“Sasa niliona nifanye surprise kwa Vanessa kwa sababu tumefanya interview sana, amekuja sana Times FM. Ila January 22 niliifanya special kwa ajili ya uchambuzi wa album yake ya kwanza ya Money Mondays huku nikiwa nimeandaa plaque hiyo (tauni) na kumpongeza kwa kutambua kazi zake.”

Ameendelea, “Plaque hiyo imepokelewa vizuri sana na wadau na lengo la kipindi na mtangazaji ni kupongeza na kuendeleza kuwapa nguvu wasanii waliofanya vizuri. Lengo langu na furaha yangu ni kubadili muelekeo na kuhamasisha kiwanda cha burudani Tanzania kutambua kazi za wasanii na kusapoti sanaa yetu kama kiwanda kinachotoa ajira kwa vijana na kuchangia pato la Taifa.”

“Furaha yangu na kazi yangu ni kusukuma muziki wetu mbele zaidi na kwa ukubwa unaostahili katika nafasi yangu.” alisema Omary Tambwe aka Lil Ommy mtangazaji wa kipindi hicho ambaye amekuja na wazo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents