Burudani

Vanessa Mdee kuachia albamu mpya chini ya Universal Music Group

Baada ya dhiki ni faraja. Vanessa Mdee afunguka kuachia albamu yake mpya mwakani chini ya Universal Music Group.

Vee Money amesema hilo baada ya kutangaza kusaini mkataba na kampuni hiyo kubwa ya muziki duniani ambayo itakuwa inasimamia kazi zake katika Ulaya na Afrika.

Akiongea na Social Buzz ya Clouds TV, muimbaji huyo amesema albamu hiyo itatoka mwezi wa sita mwakani chini ya kampuni ya Universal ambapo kwa mkataba wa aina yake ambao amesaini unamfanya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kupata dili nono kama hilo katika kampuni hiyo.

Msanii mwengine wa Bongo Flava ambaye anafanya kazi na kampuni ya Universal ni Diamond Platnumz.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents