Burudani

Vanessa Mdee kuhusu Jux, ‘alikuwa na vitabia vya ajabu ajabu’

Baada ya kutemana na mpenzi wake Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amesema sababu kubwa ya kuachana na Jux ni kutokana na tabia zake ndogo ndogo ambazo aliona kwa baadae zingemuumiza zaidi.

Picha inayohusiana
Vanessa Mdee

Vanessa Mdee amesema alikuwa anamtumia meseji asubuhi na anaona ujumbe umefika ila haujibiwi anakuja kujibu mchana na jibu lenyewe ni kwa kifupi tuu so akaona ni heri akae chonjo.

Unajua kuna tabia za kisela unakuta meseji inatumwa saa 12 asubuhi  jibu unakuja kupata saa 6 mchana na zile tiki unaziona zinakuwa za blue inakuwaje sasa?… au mtu unamuuliza umekula? yeye anajibu kwa kuguna….. yanaweza kuwa sio mapenzi ya kisela ila vile vitabia tabia vinaashiria kuna kitu,“amesema Vanessa Mdee kwenye kipindi cha Chill na Sky.

Hata hivyo Vanessa Mdee amesema hana tatizo lolote na Jux na bado anampenda kama rafiki yake kwani hawana tofauti zozote na anaamini hata Jux anampenda pia.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents