Burudani

Vanessa Mdee kutokea kwenye jarida maarufu la Marekani la Essence, August mwaka huu

Vanessa Mdee anazidi kupaa juu na kuitangaza zaidi Tanzania kwenye ramani ya muziki wa dunia.

11218931_10153390783784600_5455211341544129128_n

Hitmaker huyo wa ‘Nobody But Me’, atakava jarida maarufu la nchini Marekani, Essence Magazine.

Crew ya jarida hilo yenye takriban watu 10 wakiwemo wahariri, waandishi, watu wa make-up na mitindo imetua wiki hii na kuanzia ziara yao kwa kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti.

11333352_706219449510698_147637104_n
Crew ya Essence Magazine ikiwa kwenye mbuga ya wanyama wa Serengeti

Timu hiyo Ijumaa hii iliwasili visiwani Zanzibar ambako iliongoza na Vanessa Mdee atakayetokea kwenye jarida hilo pamoja na picha zingine.

hhh
Crew ya Essence ikiwa pamoja na Vanessa Mdee na Millen Magese

Essence wemeelezea kufurushwa na mtindo wa Vanessa pamoja wimbo wake mpya, Nobody But Me. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Essence wameandika:

“And we’re off to shoot at The Residence in Zanzibar (@trzanzibar) on Kizimkazi Beach. Our East Africa trip liaison Jill Bishop suggested Tanzania singer and DJ Vanessa Mdee (@vanessamdee) for our issue. We were instantly impressed with Vanessa’s (aka VeeMoney) style and vibe–not to mention hooked by her new song, “Nobody but Me.” We’re amped she’s here.”

Naye Millen Magese ambaye ni mmoja wa wenyeji wa crew hiyo aliandika kwenye Instagram: And you learn Swahili so fast @epezeemoji Welcome to Tanzania @essencemag . Thank you for choosing Tanzania as part of your Global Issue #BeProudTanzania We are making history #KaribuSana @essencemag #feelinghonored to be part of this .thank you for booking me and im glad I made it.”

Bongo5 imeongea na Vanessa Mdee ambaye amethibitisha kuwa location akipigwa picha kwaajili ya jarida hilo japo hajasema kama atakuwa juu ya kabisa ya jarida hilo ama atakuwa ndani. Vee Money ataonekana kwenye jarida la mwezi August linaloangazia dunia nzima.

Chini ni jarida la Essence la mwezi huu.

29561E9E00000578-3110297-image-a-1_1433378487938

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents