Burudani

Vanessa Mdee kutumbuiza jukwaa moja na Awilo, Iyanya, Burna Boy, Nigeria mwezi ujao

Miongoni mwa wasanii wa muziki wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa hapa Tanzania ni pamoja na Vanessa “Vee Money” Mdee. Juhudi zake zimemsababisha kwa muda mfupi aliokuwepo kwenye muziki kuanza kupata deals kubwa za makampuni, matangazo, na video zake kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya TV za nje na sasa milango ya shows za nje inaendelea kufunguka.

Vanessa Mdee

Vee Money ambaye video ya wimbo wake ‘Hawajui’ imekamata nafasi ya kwanza kwenye Top Ten East ya SoundCity Tv ya Nigeria, anatarajia kutumbuiza kwenye tamasha la ‘Gidi Culture Festival’ litakalofanyika April 4, 2015 jijini Lagos, Nigeria.

Twitter alipost:
vee

Kupitia Instagram ameandika:

“Nimepata nafasi ya kutumbuiza Lagos, Nigeria na kuwakilisha #Tanzania #GoodEngineering #Money15”

Miongoni mwa wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni M.I, Burna Boy, Awilo, Iyanya Waje, Victoria KImani na.

Hii si mara ya kwanza kwa Vanessa kupata shavu la show Nigeria, December 2013 aliwahi kupanda jukwaa la show kubwa Nigeria iitwayo ‘Rhythm Unplugged’ ambayo hufanyika kila mwaka na kukutanisha wasanii wa A-List wa Naija kwenye jukwaa moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents