Burudani

Vanessa Mdee: Yes every international collabo means more money in the bank (Exclusive)

Vanessa Mdee amesema collabo za kimataifa anazofanya hupeleka neema pia kwenye akaunti yake ya benki.

Siku za hivi karibuni amesikika kwenye nyimbo tatu alizoshirikishwa na wasanii mbalimbali akiwemo Orezi wa Nigeria na Tay Grin wa Malawi.

Alikuwa akijibu swali langu nililomuuliza, “collabo hizi kwa upande wako kwa namna yoyote zinamaanisha ‘more money in the bank pia?

“Yeah collabo hizi definitely zinaamisha more money in the bank,” anasema.

“Sababu kama mimi Malawi nilikuwa sijawahi kwenda kufanya show sasa hivi nimeshakaribishwa kwenye matamasha mbalimbali so more money in the bank. Pamoja na Nigeria, kesho kutwa naenda kufanya show Gidi Fest, ni tamasha kubwa, nilishawahi kufanya lakini sasa hivi nina content nyingi zaidi ambazo zina wasanii wa Kinaijeria so nyimbo zinakuwa zinafahamika na mashabiki wengi zaidi huko so definitely more money in the bank because to me every fan is a blessing na wanaendeleza muziki wangu wanaufikisha pande ambazo hata mimi sijawahi kufika,” ameongeza Vanessa.

Hata hivyo Vanessa amesema hajaishia hapo, nyingine zipo njiani.

“Nataka niattack kila nchi, ndani na nje ya bara la Afrika.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents