Michezo

VAR yashindwa kufanyakazi ghafla na kuzua utata baada ya mtumishi wa uwanja kuchomoa pini na kuchaji simu yake 

Mfanyakazi mmoja wa uwanja wa soka nchi Saudi Arabia amesababisha mfumo wa ‘Video Assistant Referee’ (VAR) kushindwa kuendelea kufanya kazi kwa muda wakati ulipohitajika kurua kipande cha video ili kutafuta kosa lilifonywa na mchezaji hii ni baada ya mtumishi huyo kuchomoa pini moja wapo na kuchaji simu yake ya mkononi.

Image

 

Mtumishi huyo alichomoa kipini katika mfumo huo wa VAR na kuchomeka simu yake chaji wakati wa mchezo wa ligi ‘Saudi Pro League’ baina ya Al-Nassr dhidi ya Al-Fateh na kusababisha sitofahamu.

Katika mchezo huo uliyokuwa wavuta nikuvute ulishuhudiwa Al-Nassr  ikichomoza na ushindi mwembamba wa bao 1 – 0 dhidi ya hasimu wake klabu ya Al-Fateh dakika ya 49 kupitia kwa mshambuliaji wake kinda mwenye umri wa miaka 19, Firas Al-Buraikan.

Mbali na ushindi huo klabu ya Al- Nassr ipo katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ‘Saudi Pro League’ ikiwa na pointi nane (8) wakati timu ya Al- Fateh inaburuza mkia nafasi ya 16 ikiwa na alama yake moja tu, wakati Al – Hilal ikiongoza kwakuwa na pointi 16.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents