Burudani ya Michezo Live

Venezuela yasitisha matangazo ya shirika la utangazaji la Deutsche Welle nchini humo

Ujerumani inawashinikiza maafisa nchini Venezuela kubadilisha uamuzi wao wa kusitisha matangazo ya kituo cha kimataifa cha televisheni cha Deutsche Welle cha Ujerumani kwa lugha ya Kihispania.

Deutsche Welle imesema juzi Jumapili kwamba matangazo hayo yameondolewa hewani na kuitaka mamlaka ya utangazaji ya Venezuela Conatel kurudisha matangazo hayo hewani.

Hapo jana siku ya Jumatatu, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Maria Adebahr amesema uamuzi wa Venezuela unasikitisha sana na kudokeza kwamba uhuru wa habari na maoni, vina thamani kubwa kwa serikali hii ya Ujerumani.

Conatel haikutoa taarifa yoyote juu ya kwanini imeondoa matangazo hayo ya Deutsche Welle kwa lugha ya Kihispania kutoka katika huduma zake.

Ujerumani ni moja kati ya nchi iliyomtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaido kuwa rais wa mpito wa Venezuela.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW