Michezo

Venus Williams atinga nusu fainali US  Open

Mcheza tenis raia wa Marekani, Venus Williams amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani (US Open) baada ya kumshinda mpinzani wake Petra Kvitov.

Venus Williams ambaye ni dada wa mchezaji tenisi Serena Williams amefanikiwa kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya seti 6-3 3-6 7-6 (7-2) usiku wa kuamkia leo Jumatano.

Hii ni kwa mara ya 23 kwa Williams mwenye umri wa miaka 37 kutinga nusu fainali ya michuano mikubwa ya Grand Slam.

Mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua hiyo, Venus Williams amesema kuwa amefurahishwa na ushindi aliyo upata huku akisisitiza kuwa bado anakabiliwa na michezo migumu mbele yake.

Wiiliam anatarajia kucheza na mwanadada, Sloane Stephens katika mchezo ujao.

Venus Williams anashika nafasi ya tisa ya katika viwango vya ubora wa mchezo huo ulimwenguni huku akifanikiwa kunyakua taji hilo la US Open kwa mara ya mwisho mwaka 2009.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents