Michezo

Venus Williams atoa chozi katika mahojiano (Video)

Baada ya wiki chache Venus Williams kuripotiwa na mafisa wa kituo cha polisi cha Palm Beach Gardens mjini Florida kuhusika kumgonga na gari mzee mwenye miaka 78, mcheza tenesi huyo amejikuta akitoa chozi mbele ya kamera kwa kujutia tukio hilo.

Venus ambaye alikuwa mshindi wa Wimbledon Open, alijikuta akitoa machozi baada ya kuulizwa swali na kituo cha runinga cha ABC News, kuhusiana na tukio hilo “There are no words to say how devastating it is. I’m completely speechless” alisema Venus kabla ya kushindwa kuaendela kuaongea.

Maafisa wa polisi katika kituo hicho walimlaumu mwanadada huyo kusababisha ajali inayoonekana kuwa ni uzembe wakati alipokuwa akiendesha gari.

Mzee huyo aitwaye Jerome Barson alifariki muda mchache baada ya kufikishwa hospitali baada ya gari alilokuwepo na mkewe kugongwa na mchezaji huyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents