Burudani

Vera Sidika ajibu mapigo kwa Huddah Monroe

Vera Sidika ameamua kujibu mabigo kwa hasimu wake wa muda mrefu, Huddah Monroe kupitia biashara yake mpya.

Vera ameingiza bidhaa inayofanana na majani ya chai kwa ajili ya kusaidia kupunguza mafuta yasiyo na kazi mwili. Uzinduzi huo umefanyika huko Kenya ambapo eneo lililofanyikia sherehe hizo lilipambwa kwa rangi za kijani na nyeupe huku mrembo huyo mwenye umbo matata akivalia gauni linalochora mwili wake.


Picha ya cover la bidhaa ya Lipstick ya Huddah Monroe

Mrembo huyo anayewatoa udenda vidume wengi ameonekana kama amejibu mapigo kwa Huddah baada ya hasimu wake huyo kuzindua bidhaa ya Lipstick mwaka jana na inaonekana kupata mafanikio makubwa nchini humo kwa kununuliwa zaidi.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents