Michezo

Victor Wanyama autaja wimbo wa Bongo Flava anaoukubali

Mchezaji wa klabu ya soka ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Kenya, Victor Wanyama, ameutaja wimbo wa Bongo Flava ambao anaupenda kwa sasa.

Akiongea katika kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM, Wanyama ameutaja wimbo huo ni Orugambo wa Saida Karoli.

“Nafuatilia sana Bongo Flava na wasanii wote wanafanya vizuri kwasasa na nimependa wimbo huu mpya wa ‘Orugambo’ wa Saida Karoli,” amesema mchezaji huo.

Wanyama pia amefunguka kuwa alikuwa na nafasi kubwa ya kujiunga kuichezea Manchester United lakini dili hilo lilikuja kufeli baada ya Sir Alex Ferguson alipotangaza kustaafu kufundisha soka mwaka 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents