Michezo

Victor Wanyama kuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita baada ya FA kumfungia

Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya na kiungo wa Southampton ya Ligi Kuu ya England, Victor Wanyama atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita baada ya FA ya England kumfungia mechi tano kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya West.
Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa Wanyama mwenye umri wa miaka 24 kuonyeshwa kadi nyekundu msimu huu, anaongezewa mechi mbili za kukosa baada ya rafu aliyomchezea Dimitri Payet.

30F2821C00000578-0-image-a-50_1454966924113

Victor Wanyama alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Bournemouth mwezi Novemba na tena akaonyeshwa kadi mbili za njano dhidi ya Norwich mwanzoni mwa Januari.

Pia anakabiliwa na faini ya klabu ya kukatwa mshahara wa wiki mbili, na kocha Ronald Koeman amesema: “Hii si kadi nyekundu ya kwanza kwake, ni ya tatu, na hiyo si nzuri. Unatakiwa kujifunza kutokana na makosa yako, hivyo nitazungumza naye juu ya hilo,”amesema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents