Michezo

Victor Wanyama: Namfahamu Mbwana Samatta

Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza na timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama amesema kuwa yeye ni shabiki wa mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo kuliko Mfalme wa Barcelona, Lionel Messi.

Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza na timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama

Wanyama ambaye yupo nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza August 12 ambapo timu yake ya Tottenham ikiwa ugenini kuvaana na Newcastle.
Ameyasema hayo kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra kinachorushwa na Radio Clouds FM.

“Nawakubali wote wawili hawa ni wachezaji wa kubwa duniani na wakati mwingine naona kuwalinganisha ni ‘Unfear’ , lakini sababu mimi ni shabiki wa Madrid nasema Ronaldo, lakini hawa ni wachezaji wawili naona wako sawa, kwakuwa ni shabiki wa Madrid nasema Ronaldo.

 

Wanyama alipo ulizwa ni wachezaji gani wa Tanzania ambao yeye anawafahamu hakusita kumtaja Mbwana Samatta.

“Kwa Tanzania nawajua Mbwana Samatta namfahamu nimeona kazi zake lakini hatuja kutana, Mrisho Ngassa pia nimemsikia sikia na nimeona kazi zake kuna wengine kama Juma Kaseja lakini sijuia kama anaendelea kucheza” amesema Mchezaji huyo wa Spurs, Victor Wanyama.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents