Burudani

Victoria Kimani azungumzia mitindo na gharama anazotumia kujiweka mrembo muda wote (Exclusive)

Victoria Kimani ni miongoni mwa wanamuziki warembo Afrika na ambao kama ni kufananisha na swala mbugani basi anawindwa sana na simba wakali. Bahati mbaya si simba wote wanaobahatika kumweka kwenye himaya zao.

Nimezungumza naye exclusively kuhusu fashion na nimemuuliza maswali haya matatu:

1. Ukiangalia picha zako, hasa kwenye Instagram ni rahisi kuwa na wazo kwamba Victoria hutumia fedha nyingi sana kujiweka mrembo muda wote. Bajeti yako ikoje kwa mfano katika wiki moja?

Well, creativity is free, I actually dont spend too much money on fashion, I get many things custom made and design many things myself

Tafsiri: Ubunifu ni kitu cha bure. Kiukweli huwa situmii fedha nyingi kwenye fashion. Hupata vitu vingi vilivyotengenezwa kwaajili yangu na hubuni vitu vingine mimi mwenyewe.

2. Huwa unajifanyia make up mwenyewe?

Yes I do my own makeup most of the time unless theres a major event to do, I also do most of my own hair coloring and styling

Tafsiri: Ndiyo, mara nyingi mimi hufanya make up zangu mwenyewe labda kama kuna tukio kubwa la kuhudhuria. Pia hupaka rangi nywele zangu mimi mwenyewe na kubuni mitindo

3. Nani ambaye hukuvutia kwenye fashion?

I get inspiration from my music, It opens up my imagination to try and create looks that are unique to me. I try not to do something that other people have done recently and I go out of my way to set trends rather than follow. It is a challenge because there truly is nothinv new under the sun, but its a very big part of my brand to be original and open minded in my fashion and beauty.

Tafsiri: Hupata hamasa kutoka kwenye muziki wangu, hufungua mafikirio yangu na kujaribu na kutengeza muonekano wa pekee kwangu. Najaribu kutofanya kile watu wengine wamefanya hivi karibuni na huenda na njia yangu mwenyewe kutengeneza mitindo kuliko kufuata. Ni changamoto kwasababu hakuna kitu kipya chini ya jua lakini ni sehemu muhimu ya brand yangu kuwa halisi na kuwa na ufahamu kuhusu mtindo na urembo wangu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents