Burudani

Victoria Kimani kung’arisha uzinduzi wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, March 7

Kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm ambacho kimekuwa hewani kwa muda wa mwaka mmoja sasa, kitazinduliwa rasmi March, 7, 2014 pale Club Infinity ambayo iko Mikocheni Resort Centre (MRC), nyuma ya Shoppers Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili kamili usiku.

USIKU WA MASTAA ARTWORK_full

Uzinduzi huu umepewa jina la USIKU WA MASTAA (THE STARS NITE) kutokana na jinsi ambavyo kipindi hiki huendeshwa ambapo watu maarufu huchagua nyimbo tano wanazozipenda zaidi lakini pia hupata nafasi ya kuzungumzia mambo mbalimbali yanayowahusu ambayo jamii ingependa kuyafahamu kutoka kwao.

Katika uzinduzi huo, kutakuwa na uwepo maalum (Special Appearance) wa mrembo na mwanamuziki wa kimataifa raia wa Kenya, VICTORIA KIMANI kwaajili kuongeza shamra shamra na kuung’arisha usiku huo akiwa pamoja na watu mbalimbali maarufu wa Tanzania.

Msanii huyo wa kike anafanya vizuri Afrika, na aliwahi kufanya vizuri na kutambulika nchini Marekani na wimbo wake ‘African Girl in America’. Hivi sasa Victoria anafanya kazi za muziki nchini Nigeria chini ya label kubwa ya ‘Chocolate City’ inayosimamia kazi za wasanii kama Ice Prince, M.I na wengine.

Uzinduzi huo utapambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Tanzania akiwemo Tunda Man, Wakazi, Climax Bibo, Navy Kenzo, Meninah, Linex, Dogo Janja na wengine kibao.

Watu watakaohudhuria watapata nafasi ya kuzungumza na kupiga picha maalum na Victoria Kimani na watu mbalimbali maafurufu wanaowapenda kama vile wanamuziki, watangazaji, wanamitindo, waigizaji na wengine, ikiwa ni sehemu ya mpango waTHE PLAYLIST kuwakutanisha wasikilizaji na watu maarufu wanaosikika kwenye kipindi.

Kuhusu The Playlist:

Kipindi cha THE PLAYLIST kilianza kwenda hewani Jumapili, February 10, 2013. Na huendeshwa na Omary Tambwe maarufu kama Lil Ommy. Kipindi hiki husikika hewani kila Jumapili kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na moja jioni.

Kipindi hiki huwaalika watu maarufu kwa lengo la kusikia aina ya muziki ambao wao wanapenda kusikiliza na sababu za kusikiliza aina hiyo ya muziki, huku wakiwaburudisha mashabiki wao kwa kucheza nyimbo hizo.

Mawasiliano

Times Fm Radio

P.O.Box 71439

Dar es Salaam.

Omary Tambwe,

Brand Manager The Playlist

Email: [email protected]

[email protected]

Phone: +255 755 476167

Twitter: @LilOmmy

Facebook: facebook.com/LilOmmy

Instagram: @LilOmmy

Website: www.timesfm.co.tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents