Burudani

Victoria Kimani: Ninafuraha kufanya kazi na wanamuziki wakubwa zaidi wa Bongo Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz

Mwimbaji wa Kenya Victoria Kimani ambaye amekuwa Tanzania kwa siku kadhaa sasa akiutangaza muziki wake pamoja na kufanya collabo na wasanii wa Bongo, amezungumza maneno ya kuondoa ukungu wowote uliokuwepo hasa kuhusu yeye na Diamond Platnumz.

kimani

Victoria amepost picha aliyopiga na mastaa wawili Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz iliyosindikizwa na ujumbe huu:

“ Mafans wangu wote, nawapenda sana sana. Nafanya kazi ya muziki kwa bidii na kwa sababu yenu. Nimepiga picha na wanamuziki wengi na wakubwa sana kote duniani. Na hiyo HAIMAANISHI KUNA MAMBO MENGINE YANAENDELEA NJE ya KAZI YA MUZIKI. Kwa hayo machache, ninafuraha sana kufanya kazi na wanamuziki wakubwa zaidi wa Bongo @ommydimpoz na @diamondplatnumz kwenye single moja. Mimi ndiye msanii wa kwanza wakike kufanya single moja na hawa wawili. Tunafocus na mambo makubwa zaidi ili East Africa iende mbele kimuziki. NAWAPENDA WOTE. Mimi wenu VICTORIA KIMANI. “

Wiki iliyopita U heard ya Soudy Brown iliibua taarifa ya ugomvi uliotokea studio baina ya Abdul Naseeb aka Diamond na mpenzi wake Wema, baada ya Wema kufika studio walipokuwa Ommy na Diamond wakirecord na Victoria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents