Burudani

Victoria Kimani wa Kenya akanusha kuwa na mahusiano na Prezzo, japo walionekana waki kiss hadharani

Mapema mwezi huu (June) kuna habari zilienea kuwa mwanamuziki mrembo wa Kenya Victoria Kimani na rapper CMB prezzo walionekana waki kiss hadharani. Wait, tatizo hapa halikuwa kukiss ila issue ilikuwa ni kwamba haikuwahi kufahamika kama Vickie na Prezzo wana uhusiano ndio sababu kitendo hicho kilifanya watu waamini kuwa ‘they are an item’.

vickie

Kupitia show ya ‘Str8up Live and Loud’ Vickie ambaye ni dada wa rapper mkongwe wa Kenya Bamboo ameonesha kushangazwa na jinsi watu wanavyomuhisi kuwa na mahusiano na Prezzo, kitu ambacho amesema sio kweli na kuongeza kuwa katika maisha yake amewahi kuonana na Prezzo mara mbili tu na mara zote ni katika matukio.

Vickie amesema mara ya kwanza alikutana na Prezzo katika show ya uzinduzi wa P-Unit, na mara ya pili ni katika uzinduzi wake mwenyewe mwezi uliopita, hivyo akahimiza kuwa hana uhusiano wowote na Prezzo.

Tazama mahojiano ya Victoria Kimani katika Str8up Live and Loud

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents