Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Video: Simon Msuva atupia mawili awania kiatu cha dhahabu

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Difaa El Jadida, Simon Msuva hapo jana amefanikiwa kufunga juma la ya mabao mawili na kuisaidia timu yake kutoka sare ya 3 – 3 dhidi ya Olympique Khouribg mchezo wa ligi kuu ya nchini Morocco.

Video ya bao la pili la mshambuliaji wa kimataifa raia wa Tanzania, Simon Msuva

Sare hiyo inaifanya Difaa kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo ya Batola Pro kwa kuwa na jumla ya pointi 38 wakizidiwa alama tisa na vinara Ittihad Tanger.

Mshambuliaji huyo wazamani wa klabu ya Yanga, Msuva amefikisha jumla ya mabao nane kwenye msimamo wa ligi hiyo na kuwa miongoni mwa wachezaji wanao wania tuzo ya mfungaji bora nchini Morocco baada ya kushika nafasi ya tano.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW