BurudaniVideos

Video 5 za Bongo Flava ‘zinazotrend’, Diamond, Joh Makini wazidi kupeta

Kama ilivyokawaida kila Jumatatu  nakuletea chart ya video tano za Bongo Flava ambazo zinatrend katika mtandao wa YouTube.

Chart ya wiki hii kuna mabadiliko makubwa kwani katika video tano za wiki iliyopita zilizobaki kwenye chart ya wiki hii ni mbili tu, Diamond na Joh Makini.

  1. Rich Mavoko ft Fid Q – Sheri (pia katika trending ya Tanzania ni namba 1), wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Country Boy ft Mwana FA – Turn Up.

https://youtu.be/D4NxfbFNLDI

2. Harmonize – Sina (katika trending ya Tanzania ni namba 4) wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Joh Makini ft Davido – Kata Leta.

3. Joh Makini ft Davido – Kata Leta (katika trending ya Tanzania ni namba 17), wiki iliyopita ilikuwa namba 2, na nafasi hii ilishikiliwa na Vanessa Mdee ft Mr P (P Square) – Kisela.

4. Aslay – Baby (katika trending ya Tanzania ni namba 23), wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Diamond Platnumz – ENEKA.

5. Diamond Platnumz – ENEKA (katika trending ya Tanzania ni namba 34), wiki iliyopita ilikuwa namba 4, nafasi hii ilishikiliwa na Nandy – Wasikudanganye. 

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents