Michezo

Video: Afariki dunia baada ya kugongana na mchezaji mwenzake uwanjani

Mlindalango wa klabu ya Persela FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Indonesia, Choirul Huda amefariki dunia akiwa uwanjani baada ya kugongana na mchezaji mwenzake katika mchezo dhidi ya Semen Padang siku ya Jumapili.

https://www.youtube.com/watch?v=W90YMVbVrAU

 

Huda mwenye miaka 38 alikimbizwa katika hospitali ya Dr Soegiri siku ya Jumapili baada ya kugongana na mchezaji mwenzake kabla ya kipindi cha kwanza lakini muda mfupi baadae ilitangazwa kwamba amefariki dunia.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa daktari,  Yudistiro Andri Nugroho amesema mchezaji huyo alifariki baada ya kupata madhara makubwa kifuani.

Mchezo huo uliisha kwa Persela kuifunga Semen Padang 2-0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents