Habari

Video: African Reconnect ya Afrika Kusini yatoa elimu kwa wanawake

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Afrika Kusini, African Reconnect wamefanya mkutano wao na waandishi wa habari Jumatano hii kwenye ukumbi wa APC uliopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mafunzo kwa ajili ya elimu ya ujasiriamali ambao wamekuwa wakiutoa kwa vikundi mbalimbali vya wanawake kuanzia Mei 14.

Mkutano huo ulihudhuriwa na watu kadhaa akiwemo Muasisi wa shirika hilo, Numdeni Chengeta, Mwanamuziki mkonwe wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka, Rose Marry Jairo ambaye ni Mtumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Angella Gloria Bindo (Mratibu wa mkutano huo), Seven Mosha (Meneja wa Alikiba) na wengine.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo, muasisi wa shirika hilo ameeleza sababu ya kuanzisha mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa wanawake ili waweze kupata elimu na kuongeza uwezo wa kipato chao.

Lakini pia ameongeza kuwa ameshafanya mikutano minne mikubwa ya kutoa elimu hiyo katika nchi kama Afrika Kusini na Nigeria.

Utoaji huo wa elimu kwa vikundi hivyo vya wanawake unatarajiwa kufikia tamati Jumamosi hii ya Mei 19 ya mwaka huu kwa kutoa tuzo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents