Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Video: Aishi Manula ajipanga kuvuna pesa kwenye mitandao ya kijamii

Mlindalango namba moja wa klabu ya Simba, Aishi Salum Manula amesema kuanzia sasa atakuwa makini na mitandao yake ya kijamii ili kuhakikisha inakuwa sehemu ya chanzo kingine cha mapato, kipa huyo ameyasema hayo baada ya kupata semina ya matumizi bora ya mitandao hiyo kutoka katika kampuni ya kubashiri michezo ya SportPesa ambayo ndiyo wadhamini wa kuu wa timu hiyo.

Akizungumza na Bongo5 baada ya semina hiyo Aishi Manula amesema “Mi binafsi nilikuwa nachukulia mitandao yangu ya kijamii kama nisehemu tu ya kawaida hivyo sikuichukulia muhimu sana.” Amesema Aishi ambaye nigolikipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita.

Manula ameongeza kwa kusema “Nadhani umefika muda sasa kwa wachezaji kutumia mitandao ya kijamii kuwa sehemu ya kuwaongezea kipatao na kuwalipa mwanzoni nilikuwa naweka picha nikiwa na marafiki, ndugu na wakati mwingine nikiwa mitaani.”

“Nadhani umefika muda sasa hatapicha ambayo nitapiga nitahitaji kuwe na kamera zenye kueleweka  na hata ikiwezekana kuwepo na mtu ambaye anasimamia mitandao yako ili kuhakikisha kitu kitakachowekwa kiwe chenye mvuto na kueleweka,” amemalizia Manula.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW