Video: Aloneym ataja sababu za muziki wa Zanzibar kutotusua
Mtayarishaji wa muziki kutoka kisiwani Zanzibar, Aloneym amedai kuwa ukosefu wa menejimenti na usimamizi nzuri kumpelekea kuleta ugumu katika tasnia hiyo.
Aloneym amieleza Bongo5, kuwa muziki wa Zanzibar unaonekana mgumu kutokana na kukosa uongozi mzuri na usimamizi hafifu ndio unaofanya kuonekana kuwa hakuna wanamuziki wengi na kupelekea muziki huo kuwa mgumu kwa baadhi ya wasanii.
“Kweli Zanzibar, muziki ni mgumu na ugumu unasababishwa labda na strong management hatuna, so we need strong menegement labda muziki watu watauona. Kwa sababu hatujapata watu wenye misukumo wanaotakiwa na ndiyo maana tunaonekana tunakuwa chini daily,” amesea Aloneym.
Pia ameongeza “Wasanii wanaoonekana wanafanya vizuri ni kwa sababu wana strong management, ukimwangalia AT ni mtu ambaye ana management yake, Bell Black na wengine ndiyo maana wanakuwa wanafanya vizuri.”
Na Laila Sued na Salum Kaorata