Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Video: Auawa kwa kupigwa risasi Marekani akionekana live Facebook

Mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Prentis Robinson (55) maarufu kama Cowboy, amepigwa risasi hadi kufa wakati akijichukuwa live kwenye mtandao wa Facebook huko nchini Marekani.

Kwa mujibu wa polisi, wamesema kuwa tukio hilo limetokea karibu na chuo kikuu kilichopo Kaskazini mwa mji wa Carolina siku ya Jumatatu.

https://youtu.be/T2H-fUsPLl0

Katika video hiyo ambayo Prentis akijichukua live alionekana akiongea na mtu mwingine pembeni muda mfupi kabla ya mtu huyo kumfyatulia risasi nne ambapo milio yake imesikika kwenye video hiyo.

Hata hivyo muuaji huyo alifanikiwa kuonekana katika video hiyo na kutambulika kwa jina Douglas Colson na tayari amekamatwa na kushikiliwa na polisi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW