Burudani

Video: AY amtambulisha muongozaji wa video ya ‘Zigo’ remix, tazama ilivyokuwa wakati wa kushoot video hiyo S.A

Video ya ‘Zigo’ remix inakaribia kufikisha views milioni moja na nusu, ikiwa ni takribani wiki mbili toka ilipowekwa kwenye mtandao wa YouTube Januari 22, 2016. Bila shaka ungependa kuona yaliyojiri nyuma ya kamera wakati wa uchukuaji wa picha za video hiyo.

Ambwene Yessaya a.k.a AY ametoa video ya ‘Behind The Scene’ kutuonesha na kueleza jinsi mambo yalivyokuwa huko Afrika Kusini wakati wa zoezi hilo.

AY ambaye pia ameahidi kuwa mwaka huu atahakikisha anatoa nyimbo tano kama sio sita, ili kufidia madeni ya miaka iliyopita ambayo hakutoa nyimbo nyingi, ameanza kwa kueleza sababu za kuamua kumtambulisha muongozaji mpya, si mpya kwa maana ya kuanza kufanya kazi hiyo, bali ni mpya kwa wasanii na mashabiki wa Tanzania, kama alivyofanya na Godfather miaka kadhaa iliyopita, ambaye baada ya kuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kufanya naye video ndipo wasanii wengine wa Bongo walianza kumfata.

Wapo waongozaji wengi wa video nchini Afrika Kusini, lakini wale ambao majina yao sio mageni sana kwa ukanda wa Afrika Mashariki ni kama Godfather na Justin Campos ambaye ametokea kuvuma zaidi kuanzia mwaka jana, licha ya kuwa ni muongozaji wa siku nyingi.

Alessio
Alessio (kushoto)

Muongozaji aliyefanya video ya ‘Zigo’ remix anaitwa Alessio Bettochi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Studio Space Pictures (SSP), ambao pia wamefanya video mpya ya Mwana FA ‘Asanteni Kwa Kuja’.

“Mimi nilikuwa sijawahi kukutana na Alessio mwanzo kabla ya kufanya hii Zigo,na kitu kikubwa ambacho nilichokuwa nakiangalia, nilikuwa nakiangalia katika mazingira kuwa nimeshafanya video na Godfather, nimeibrand hiyo hali ya kwenda South Africa kushoot video na zinatoka kali, na nimependa jinsi ambavyo na watu wengine wamefata na nimefurahia jinsi ambavyo kumbe idea zangu nikifikiria kitu kikifanyika na kinafanyika nikasema no, so I think ni vizuri kama ningeweza kuintroduce na director mwingine ambaye ni Alessio.” Ameeleza AY katika clip ya BTS.

Msikilize/mtazame hapa AY akiielezea safari nzima ya ‘Zigo’ kuanzia utengenezaji wa audio (original) hadi video ya ‘Zigo’ remix.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents