Videos

Video: Azma ammdiss Nay wa Mitego kwenye wimbo wake mpya ‘Wanasubiri Nife’?

Rapper wa Tamaduni Muzik, Azma Mponda ameachia video ya ngoma yake mpya, Wanasubiri Nife. Kwenye ngoma hii, kwa uchungu Azma amezungumza kwa uchungu jinsi ambavyo anahisi watu wanamchukulia poa licha ya kuwa miongoni mwa rapper wakali Tanzania.

Anahisi watu wanasubiri afe ndio wakitambue kipaji chake. Kwenye wimbo pia, Azma amemdiss Nay wa Mitego.

“Najua mnajua kuwa najua ila hamuwezi kunichukua kwenye tour mnawachukua wasiojua ‘mitego wanayoitega’, naitegua,” anarap mkali huyo.

Azma amerap pia kuhusu jinsi asivyopenda kulumbana licha ya kuona anabaniwa hewani.

“Ingawa wachache wanabana ninafanya, ninafana ninapiga hatua, kila siku namuamini maulana, sipendi kulumbana sina laana sina dhana, ila mkiendelea kubana, kuna siku nitawatukana ili tuweze kuheshiamiana,” anasisitiza kwenye video hiyo iliyofanywa na Kinye Media ya Mwanza.

“Ninatunga tungo kali, hewani hazisikiki, ninafanya yenye amani, wanahabari hawaandiki, nimezama kwenye dhiki mpaka mashabiki wanabana, mwenye sifa sisikiki wanasikika wasiofana, mimi ni bora zaidi ya hao wanaosikika, mimi ni bora zaidi ya hao wanaosifika.”

Amerap pia kuhusu jinsi rappers wengi kuwa na majina makubwa lakini hawana kitu, na pindi wanapokufa ndipo watu hujitokeza kuonesha ufahari kwenye misiba. “Kutwa unapiga ili utoke kwenye msingi, unakuwa na jina kubwa ila kimaisha uko chini, unafanya kazi kubwa wadau hawaithamini, wanasubiri ufe wakaonyeshe ufahari kwenye msiba, hawataki upate tiba ukiwa hai.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents