Mitindo

Video: Baada ya Khadija Mwanamboka kuzindua nguo mpya ‘nitakufa nikiwa mbunifu wa mavazi’

Mbunifu wa mavazi, Khadija Mwanamboka amefuka kwa kusema kutokuoneka mara kwa mara kwenye fashion show si kwamba amesimama kazi hiyo kwani anaamini ataifanya kipindi chote cha maisha yake.

Khadija amesema hayo mwisho wa weekend iliyopitia wakati wa uzinduzi wa nguo zake mpya kwa kushirikiana na kampuni ya Nida, huku wakiongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Mapinduzi ya mitindo na ku-support Tanzania ya viwanda’

“Huwa siogopi kitu, nikitaka kitu huwa nafanya the end of the day simkwazi mtu, simkosei Mungu wangu, sivunji sheria, kwa hiyo namshukuru Mungu kanibariki kipaji. Mimi ni mbunifu nitakufa nikiwa mbunifu wa mavazi” amesema.

“Sasa Watanzania wakiwa hawakuoni kwenye fashion show wanasema Khadija siku hizi hashoni nguo, no!!! , hata ukienda popote duniani utambulisho wangu ni mbunifu hata niuze almasi bado Khadija atabakia kawa mbunifu” ameongeza.

Pia amesema kuwa nguo hizo zipo kwa ajili ya rika zote na licha ya kuuzwa hapa nchini amejipanga kuuza katika nchi za Marekani, German na Italy.

“Nataka niwafikie Watanzania wengi kwa malengo mawili, kwanza wawe na nguo zangu nifaidike kama mbunifu na vile vile wachukue fursa waziuze kwa bei iliyochini sana na nimejaribu kumfikiria kila mtu” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents