Burudani

Video: Baada ya kutohudhuria BET kisa ujauzito, Card B aelezea ushindi wake

Rapper wa kike kutoka nchini Marekani, Card B amewashukuru mashabiki wake na kila mmoja kufuatia ushindi alioupata kwenye tuzo za BET 2018.

Tuzo hizo ambazo zilitolewa usiku wa kuamkia leo June 25, 2018 Los Angles nchini Marekani, Card B alishindwa kuhudhuria kutokana na ujauzito alionao kwa sasa.

Jambo hilo lenye kheri katika maisha yake halikumzuia kushinda tuzo ya Best Female Hip Hop Artist Award, Pia ameshinda katika kipengele cha Best Collaboration Award kupitia ngoma yake ‘Bartier Cardi’ aliyomshirikisha 21 Savage. Hata hivyo Card B ameeleza kuwa wanawame wanaofanya muziki wa Hip Hop hawapewi support kama inavyotakiwa.

Katika ushindi huo wa BET 2018, Card B amewabwaga wasanii kama Remy Ma, DeJ Loaf, Rapsody na Nicki Minaj. Huu ni mwaka nzuri kwa Card B kwani April, 2018 ndipo aliachia albamu yake ‘Invasion of Privacy’ ambayo ndani ya siku sita sokoni iliweza kufika mauzo ya Gold (kuuza copy zaidi ya 500,000).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents