Burudani

Video: Baada ya rafiki yake kuuawa na watu wasiojulikana, Drake ahudhuria maziko

Msanii kutoka nchini Marekani, Drake alihudhuria katika maziko ya rafiki yake , Anthony Soares “Fif” ambaye aliuawa kwa kupingwa risasi na watu wasijulikana katika mji waToronto nchini Canada.

Drake na Soares

Drake alihudhuria mazishi ya Soares Jumamosi ya weekend iliyomalizika ambayo yalifanyika katika jumba la Ogden Funeral Home huko Scarborough na baadaye mwili wa Soares ulisarishwa hadi kwenye makaburi ya Duffin Meadows kwa ajili ya maziko.

Watu waliohudhuria katika mazishi hayo wamesema hata hivyo Drake hakuzungumza chochote na muda mwingi alipenda kujitenga na maandamano ya watu.  Kwa mujibu wa video ya mtandao ya TMZ Drake alikuwa beka kwa beka hadi pale mwili wa Soares unashushwa kwenye kaburi.

September 15 mwaka huu kupitia mtandao wa Instagram Drake alielezea kuguswa na kifo cha Soares na kueleza ni kitu asichoamini kama kweli kimetokea kwani walishirikiana kwa miaka mingi.

Soares aliuawa kwa kupingwa risasi na watu wawili wasiojulikakana, hata hivyo polisi wametoa video ya wauwaji ya waliotekeleza mauaji hayo na hakuna aliyetiwa nguvuni hadi sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents