Burudani

Video: Bado nahitaji kusaidiwa na WCB – Q Boy

Aliyekuwa mtu wa mitindo wa Diamond na WCB mzima ambaye kwa sasa ameingia kwa miguu miwili kwenye muziki, Q Boy Msafi, amewataka wadau wa muziki kuacha kumgombanisha na WCB kwa kuwa bado anahitaji msaada mkubwa kutoka ndani ya label hiyo.

Q Boy alifukuzwa ndani ya label hiyo baada ya kudaiwa kumruhusu shabiki kupiga picha mbele ya gai la Zari ambaye ni mama watoto wa Diamond.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Boy amedai kuna watu wanatengeneza mazingira ili tatizo lake na WCB lionekane kubwa.

“Muziki siyo vita ujue, muziki ni kitu ambacho hauwezi kufanya bila kuomba msaada wa wadau wako wa karibu. Bado nahitaji msaada wa WCB, kesho nitakuwa na kazi ambayo nitahitaji kufanya kolabo,” alisema Q Boy.

Aliongeza, “Kwahiyo ninavyosikia watu wanazungumza vibaya kuhusu mimi na WCB najisikia vibaya kwa sababu mimi bado nahitaji msaada wao. Hata kazi zangu zilizopita wao walikuwa mstari wa mbele kunisaidia,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents