Video: Bahati aeleza mazito kuhusu show yake aliyojaza uwanja Kenya na kuweka rekodi

Cassper Nyovest amekuwa na rekodi zake mbili tofauti za kujaza viwanja vikubwa vya mpira wa miguu nchini Afrika Kusini kwa kuandaa show zake mwenyewe. Bahati kutoka Kenya amekuwa msanii wa kwanza nchini humo kufanya hivyo na kujitengenezea rekodi ya muziki wake.

Bahati alifanya show hiyo usiku wa Disemba 31 mwaka jana katika uwanja wa mpira wa miguu, Thika Stadium. Akiongea na mwandishi wetu Teddy Agwa, msanii huyo amesema kitu hicho kilikuwa ni kipya nchini Kenya kwa kuwa wasanii wenyewe wamekuwa wakiogopa kufanya hivyo na badala yake wamekuwa wakisubiriwa kuitwa kwenye show na mapromota.

Bahati ameongeza kuwa wakati anataka kufanya show yake hiyo alikuwa amealikwa kufanya show nyingi sana kwenye tarehe kama hiyo na pia alikuwa anawaza show yake inaweza ikaharibika kwa kutopata watu wengi.

Muimbaji huyo amesisitiza kuwa mwaka huu mipango yake ni kufanya show kwenye viwanja pekee.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW