Burudani

Video: Barakah The Prince awachana wasanii wenzake, amtaja Alikiba, Dimpoz na Diamond

Msanii Barakah The Prince ameamua kuwachana wazi wasanii wenzake kwa kuwatolea mifano Alikiba na Ommy Dimpoz lakini pia amempongeza zaidi Diamond Platnumz.

Akiongea na Bongo5, Barakah amesema, kwa msanii ili aonekane ni mkubwa zaidi kitu cha kurudia nguo ni mbaya sana kwa kuwa inamuharibia brand yake hasa anapokuwa kwenye interview au wakati wa kushoot video.

“Kwa mfano Bongo kwa mtu kama Ommy Dimpoz, Ommy ni package kabisa ya staa, Diamond ni package na Alikiba ni package iliyokabilika ambayo unaona kabisa huyu ni staa kakamilika. Kwa hiyo kwenye muonekano pia hususan mavazi na mwili lazima mtu uwe makini sana,” amesema msanii huyo.

Baraka pia amempongeza Diamond kwa jitihada zake za kujituma katika biashara na kuwaamsha watu. “Diamond ni miongoni mwa mtu ambaye anaowasanua sana watu kwenye vitu, nani alitegemea kama Diamond anaweza kuja na Chibu perfume? Hakuna mtu aliyetegemea, lakini jamaa kaka kafikiria watu wanapenda sana kunukia,” ameendelea.

“Nampongeza sana Diamond, ni mtu ambaye anatumia nafasi yake aliyopo sasa hivi vizuri. Kwa hiyo sitaki kusema kuwa watu wengi wanafanya kwa kuwa yeye kafanya, no lakini uyeye anaweza akawa anawapa watu mioyo ya kuthubutu. Unajua mtu mpaka kurizki na kuweka hela yake nyingi kwenye brand ya nguo au nini, ujue hapo umerizki na biashara ina mambo mawili, kuna kunyanyuka na kuna kuanguka.” Amesisitiza.

“Mtu mpaka uweze kurizki lazima uone mfano kwa mtu, huwezi kurizki tu, kwa hiyo yeye ni miongoni mwa watu wanaowapa watu moyo na kuona kumbe kitu hiki unaweza kukifanya na kitu hiki na kikawezekana na tukabiga mitonyo na maisha yetu yakawa mazuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents